KACHAPIN ATAKA POLISI WANAOENDELEZA OPARESHENI MARICH KUONDOLEWA MARA MOJA.


Gavana wa kaunti hii ya pokot magharibi simon kachapin ameitaka idara ya polisi kuondoa vizuizi kwenye barabara kuu ya kapenguria kuelekea lodwar akidai vinatumika visivyo na polisi kuwanyanyasa wasafiri .
Akizungumza katika eneo la kishaunet, kachapin alitaja hasa kizuizi cha marich pass kama kinachotumika visivyo na maafisa wa polisi na kumtaka inspekta mkuu wa polisi kuchukua hatua ya haraka kuondoa kizuizi hicho.
“Wale askari ambao wamemwagwa pale marich wanawahangaisha wananchi ambao wanaendeza shughuli zao za kawaida. Hatuelewi ni nani huyo ameamrisha polisi kuletwa sehemu hiyo badala wangekuwa maeneo ya mipakani kudumisha usalama wa wananchi.” Alisema Kachapin.
Aidha gavana Kachapin alitaka maafisa hao kuondolewa na kupelekwa maeneo ya mpakani pa kaunti hii na kaunti jirani ambako kuna tatizo la usalama badala ya kuwahangaisha wahudumu wa magari, boda boda pamoja na wasafiri.
“Nataka kuijuza serikali kwamba mambo yanayoendelea eneo hilo la marich sijayafurahia kama gavana wa kaunti hii. Yanafaa kuchunguzwa sana kwa sababu huenda yataleta hali ambayo si nzuri kwa kuwa watu wasio na hatia wanahangaishwa sana.” Alisema.