KACHAPIN AKOSOA HATUA YA WATUMISHI WA UMMA KUJIHUSISHA NA SIASA.

Na Benson Aswani
Aliyekuwa gavana wa kaunti hii ya Pokot magharibi Simon Kachapin ametofautiana na misimamo ya baadhi ya maafisa serikalini ambao tayari wametangaza misimamo yao ya kisiasa katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Kachapin ambaye ni katibu katika wizara ya michezo, utamaduni na toradhi za kitaifa amesema kuwa mtumishi wa umma anastahili kutekeleza majukumu yake kulingana na kiapo alichochukua bila kuegemea mirengo yoyote na kutojihusisha na maswala ya kisiasa kabla ya wakati unaoruhusiwa kikatiba.
Wakati uo huo Kachapin amedokeza mipango yake ya kugombea kiti cha ugavana katika kaunti hii ya Pokot magharibi mwaka ujao ila akisisitiza kuwa atatangaza wazi msimamo wake na chama atakachotumia punde kipindi chake cha kuhudumu katika wizara hiyo kitakapokamilika na kutangazwa rasmi kipindi cha kisiasa.

[wp_radio_player]