KACHAPIN ADAI VYAMA VINATUMIKA KUPORA MALI YA UMMA.

Na Benson Aswani

Aliyekuwa gavana wa kaunti hii ya Pokot magharibi Simon Kachapin amekosoa vikali hatua ya kubuniwa vyama vingi nchini anavyovitaja kuwa vya kikabila.
Akirejelea chama kipya cha KUP kilichizinduliwa majuzi katika kaunti hii ya Pokot magharibi, Kachapin ambaye pia ni katibu katika wizara ya michezo, utamaduni na toradhi za kitaifa amesema kuwa hatua ya kubuniwa vyama kila mara nchini inawachanganya zaidi wananchi.
Kachapin anadai kuwa baadhi ya viongozi wanaobuni vyama hivi wanatumia fedha za umma kuendesha shughuli za vyama hivyo pamoja na zao za kibinafsi huku akitaka kuanzishwa uchunguzi wa kila kiongozi kubaini kiwango cha mali walicho nacho.
Aidha Kachapin amedai kuwa ipo miradi ambayo imetelekezwa katika kaunti hii ya Pokot magharibi ikiwemo barabara ambazo zipo katika hali mbaya hali hamna anayeishughulikia huku wahusika wakijihusisha pakubwa na kujinufaisha kupitia mali ya umma.