KACHAPIN AAHIDI KUBADILISHA SURA YA POKOT MAGHARIBI.


Kaunti ya pokot magharibi imepata sura mpya baada ya Gavana mteule wa kaunti hii ya Pokot magharibi Simon Kachapin kuahidi kuhakikisha kuwa anatumia miaka mitano ambayo amekabidhiwa kuongoza kaunti hii kuimarisha maisha ya wakazi kwa kuhakikisha kuwa uchumi wa kaunti hii unaimarika.
Akizungumza katika hafla ya kurudisha shukrani kwa wakazi baada ya kuchaguliwa kuonghoza tena kaunti hii, Kachapin amesema kuwa ataziba mianya ambayo imekuwepo katika uongozi wa gavana anayeondoka John Lonyangapuo anayodai imetumika kuwapunja wakazi.
Ametaja shirika la WEPESA kuwa moja ya sehemu ambazo analenga kufanyia marekebisho kuhakikisha kuwa mkazi wa kaunti hii hapitii wakati mgumu kuendesha shughuli zake za kila siku.
Wakati uo huo Kachapin amewataka wakazi wa kaunti hii kuendelea kudunisha amani hata wanaposubiri matokeo ya urais kutangazwa na tume ya uchaguzi IEBC, akiitaka pia tume hiyo kutenda haki kwa kuhakikisha kuwa rais aliyechaguliwa na wananchi anatangazwa.