JUHUDI ZA KUOKOA MAPENDEKEZO YA BBI HUENDA ZIKAELEKEZWA BUNGENI.


Juhudi za kuhakikisha baadhi ya mapendekezo muhimu ambayo yalikuwa yakishinikizwa kupitia mpango wa upatanishi BBI uliotupiliwa mbali na mahakama kuu na kisha ile ya rufaa sasa zitaelekezwa katika bunge la taifa na lile la seneti.
Akizungumza na kituo hiki seneta wa kaunti hii ya Pokot magharibi Samwel Poghisio amesema kuwa mchakato wa BBI ulikuwa na manufaa makubwa kwa ustawi wa magatuzi na kuwa hatua ya kutupiliwa mbali na mahakama ni pigo kubwa kwa taifa.
Amepuuzilia mbali madai kuwa mchakato wa BBI ulilenga kuwanufaisha baadhi ya viongozi nchini, akielezea hofu huenda baadhi ya maeneo bunge yenye idadi ya chini ya watu yakafutwa kinyume na ilivyokuwa ikipendekeza BBI kuongezwa idadi ya maeneo bunge.
Wakati uo huo Poghisio amemshutumu naibu rais William Ruto ambaye mrengo wake umekuwa msitari wa mbele kupinga mchakato wa BBI kwa kile amesema kumkosea heshima kiongozi wa nchi kwa kupinga maamuzi yake swala ambal o ni kinyume na majukumu yake kama naibu rais.