JUHUDI ZA KUKABILI UKEKETAJI BARINGO ZAPONGEZWA


Viongozi pamoja na wanaharakati wa kutetea haki za watoto eneo bunge la Tiati kaunti ya Baringo wameelezea kuridhishwa na hatua zilizopigwa katika kukabili ukeketaji.
Wakiongozwa na mwakilishi wadi ya Loya Moroko Maria Losile, viongozi hao wamesema kuwa utamaduni huo umekabiliwa kwa asilimia kubwa baada ya wakazi wengi kukumbatia elimu ya mtoto wa kike.
Japo amesema kuwa kuna baadhi ya sehemu ambazo zingali zinashuhudia visa hivyo, Losile amesema ushirikiano wa wadau mbali mbali ikiwemo waathiriwa wa visa hivyo umepelekea kukabiliwa utamaduni huo kwa kiwango kikubwa.