JOSHUA KUTUNY APONGEZA JUBILEE KWA KUMTEUA KAMA NAIBU KATIBU MKUU WA CHAMA HICHO


Naibu katibu mkuu mpya wa chama cha Jubilee Joshua Kutuny amepongeza chama hicho kufuatia uteuzi wake katika nafasi hiyo baada ya mbunge wa Soy Caleb Kositany kutimuliwa.
Akizungumza na wanahabari katika shule ya upili ya Nyakinyo kwenye kaunti ya Trans Nzoia alipokuwa anapokeza shule hiyo basi Kutuny amesema kuwa atatumia nafasi hiyo kuimarisha demokrasia chamani.
Kutuny kadhalika amesema kuwa uteuzi wake ni heshima kubwa kwa wapiga kura wake na wakenya wanaoshabikia amani na umoja wa kitaifa.
Kutuny hata hivyo amesema kuwa atatumia fursa hiyo ili kupigia debe mchakato wa BBI kikamilifu.