JOHN MENGWA AJIONDOA KWENYE KINYANG’ANYIRO CHA UBUNGE SABOTI TRANS NZOIA.


Mgombea kiti cha eneo bunge la Saboti kwa tiketi ya chama cha UDA John Meng’wa amejiondoa kwenye kinyanganyiro hicho.
Akihutubu kwenye hafla iliyo waleta pamoja viongozi wa jamii na wazee ya jamii ya Sabaot kutoka eneo bunge hilo, Mengwa amesema ametangaza kujiondoa kwenye nafasi hiyo na badala yake kutafuta uongozi kwenye nyadhifa tofauti ya kuwa hudumia wenyeji wa Kaunti ya Trans Nzoia.
Ni hatua ambayo imeungwa mkono na Baadhi ya viongozi kutoka kaunti ya Trans Nzoia wakiongozwa na aliyekuwa mgombea mwenza Jonas Kuko
Wakati uo huo mshirkiksihi wa chama cha UDA eneo bunge la Saboti Charles Samoei amekariri kuendelea na mazungumzo na viongozi zaidi ili kutoa nafasi ya chama cha UDA kujinyakulia viti vingi zaidi kwenye uchaguzi mkuu ujao.