JOEL ONGORO ATIMULIWA KAMA KIONGOZI WA WENGI KATIKA BUNGE LA KAUNTI YA KAKAMEGA


Jumla ya wawakilishi wadi 69 kati ya 89 wa bunge la kaunti ya Kakamega wamemtimua kiongozi wa wengi Joel Ongoro kutoka kwa wadifa huo kutokana na mzozo wa uongozi unaoshuhudiwa katika bunge la kaunti hiyo.
Wawakilishi wadi hao pia wamemuondoa Ongoro kutoka kwa bodi ya bunge hilo kwa madai ya ubadhirifu wa fedha na kushindwa kushughulikia ipasavyo maslahi ya wawakilishi wadi hao kwa bodi.
Kulingana na wawakilishi wadi hao ni kwamba hatua yao haijashinikizwa kisiasa.