JLAC YATAKIWA KUELEZA KUHUSU MISWADA MIWILI TOFAUTI YA BBI

Mbunge wa kiminini kaunti ya Trans nzoia Dkt Chris Wamalwa ametoa wito kwa kamati ya haki na sheria kujitokeza wazi na kuwaeleza wakenya kilichosababisha mikanganyiko katika miswada iliyowasilishwa mbele ya bunge la taifa na seneti.
Wamalwa amesema kuwa ni kinyume na sheria kufahamu kuwa bunge la senti ndilo lililo na mswada sahihi wa bbi kutoka kwa tume ya uchaguzi na mipaka iebc huku la kitaifa likiwa na mswada ambao ni tofauti kabisa.
Yanajiri haya huku mkanganyiko ukiibuka kuhusu tarehe rasmi ya vikao maalum vya kujadili ripoti ya kamati ya pamoja ya haki na sheria kuhusu mswada wa marekebisho wa katiba wa mwaka 2020.
Kiongozi wa wengi katika bunge la taifa Amos Kimunya amesema kuwa spika wa bunge hilo Justine Muturi atatangaza leo siku rasmi ya vikao hivyo.