JANGA LA CORONA LAATHIRI UTEKELEZWAJI WA MIRADI TRANS NZOIA.


Athari za janga la corona zimeathiri pakubwa utekelezaji wa miradi mbali mbali serikali kanda bonde la ufa.
Akizungumza kwenye soko la Kolongolo katika kaunti ya Trans nzoia, mshirikishi wa utawala eneo la bonde la ufa George Natembeya amesema kuwa miradi hiyo ni pamoja na barabara ya kilomita 60 ya kutoka Lesos, Namanjalala, Kolongolo na Chepchoina ya kima cha shilingi bilioni 2.3.
Aidha kuna mradi wa Kitale, Endebes, Swam wa kima cha shilingi bilioni 4.5, na ule wa maji wa Kolongolo Kiptogot wa shilingi bilioni 1 ambao utafaidi zaidi ya familia laki mbili kupata maji safi na salama ya matumizi.
Kuhusu maswala ya elimu Natembeya amewaonya vikali wakuu wa taasisi za elimu ambao wanatuma wanafunzi nyumbani kufuatia ukosefu wa karo.