JAMII YATAKIWA KUZINGATIA MTOTO WA KIKE KATIKA ELIMU POKOT MAGHARIBI.
Mtoto wa kike kaunti hii ya Pokot magharibi anastahili kupewa kipau mbele na jamii hasa katika maswala ya elimu.
Haya ni kwa kujibu wa afisa katika shirika la Yang’at Elizabeth Kukat ambaye amesema kuwa japo mtoto wa kiume anafaa kuzingatiwa, mtoto wa kike ndiye anayekabiliwa na changamoto tele katika jamii kuliko Yule wa kiume ikiwemo ukeketaji, pamoja na shughuli mbali mbali za nyumbani.
Aidha Kukat amepongeza jamii kwa ushirikiano na shirika hilo pamoja na wadau wengine katika kuhakikisha mazingira bora kwa mtoto wa kike hasa kwa kuchangia katika ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya msingi ya chepakul, huku akiwahimiza kuendelea kukumbatia masomo kwa wanao.