JAMII YA TOROIS KAUNTI YA BARINGO YADAI KUTENGWA NA SERIKALI.


Viongozi kutoka jamii ya Torois katika kaunti ya Baringo wanadai kutengwa na serikali kuu pamoja na ile ya kaunti huku watu wa jamii hiyo wakiendelea kupitia matatizo mengi.
Christine kandie ambaye ni mmoja wa viongozi wa jamii hiyo amesema kuwa wanapitia changamoto nyingi kama vile utovu wa usalama unaoambatana na visa vya wizi wa mifugo, ukame na mafuriko hasaa wakati wa msimu wa mvua.
Kandie anasema kuwa licha ya matatizo hayo yote, hawajapata msaada wowote kutoka kwa serikali kuu ambapo sasa ameelezea haja ya viongozi wa jamii hiyo kuhusishwa kwenye harakati ya kutatua baadhi ya changamoto zinazowakumba wakazi.