JAMII YA SENGWER YALALAMIKIA KUTENGWA KATIKA UONGOZI.

Na Benson Aswani
Jamii Ndogo ya Segwer wanaoishi kwenye Kaunti za Pokot Magharibi na Trans-Nzoia sasa wanataka kifungu cha katiba cha 57 kinacholinda jamii ndogo kutekelezwa kikamilifu ili kulinda haki ya jamii ya walio wachache humu nchini.
Wakihutubu katika wadi ya Siyoi eneo bunge la Kapenguria wasomi kutoka jamii hiyo wakiongozwa na David Kiptum wametaka jamii hiyo kupewa nafasi na jamii ya pokot wanaoishi katika wadi hiyo kuwania kiti cha wadi ya Siyoi kwani ni maeneo hayo pekee ndio jamii hiyo inapatikana kwa wingi Katika Kaunti hii ya Pokot Magharibi, ili kuipa jamii hiyo nafasi ya uwakilishi katika bunge la Kaunti.
Kwa upande wake wakili Justus Kiprop ameelezea haja ya nafasi za uteuzi katika mabunge ya kitaifa zilizotengewa jamii za walio wachache kuheshimiwa, akilalamikia hatua iliyopelekea kwa jamii ya Ogiek kupewa nafasi hiyo hali idadi yao ni kubwa nchini kuliko jamii ya segwer, huku wakitoa wito kwa umoja wajamii hiyo.