JAMII YA SABAOT TRANS NZOIA YAJITENGA NA MATAMSHI YA UCHOCHEZI YA KIONGOZI MMOJA KUTOKA JAMII HIYO.


Jamii ya Sabaot Kaunti ya Trans Nzoia ikiongozwa na Francis Muneria Chemonges imejitenga na matamshi ya uchochezi yanayodaiwa kutolewa na Mwakilishi Wadi mteule katika Wadi ya Machewa hivi majuzi huku vitengo vya usalama vikitakiwa kuwachukulia hatua kali za kisheria wanasiasa kama hao.
Akiongea na wanahabari katika Wadi ya Machewa Muneria amewarai wanasiasa kufanya kampeni zao kwa amani na kuepuka matamshi yanayoweza kutenganisha jamii mbalimbali zinazoishi maeneo hayo hasa msimu huu ambapo taifa linajiandaa kwa uchaguzi mkuu.
Juma lililopita Mwakilishi Wadi mteule katika chama cha Jubilee Everlyne Cheshari alitoa matamshi ambayo yalionekana kukera wenyeji wa Machewa katika hafla moja alipokuwa akiomba kura katika Wadi hiyo baadhi ya wakazi wa eneo hilo wakimtaka kujitokeza na kuomba msamaha au kufafanua zaidi kuhusu alichokuwa akimaanisha