JAMII YA SABAOT TRANS NZOIA YAGAWANYIKA KUHUSU NAIBU GAVANA WA KEN LUSAKA.


Viongozi wa jamii ya sabaot katika kaunti ya Trans nzoia wameshindwa kuafikiana kuhusu ni nani anayepaswa kuteuliwa kuwa naibu gavana wa Ken Lusaka kwenye uchaguzi mkuu ujao kwa madai ya kuachwa nje kwa jamii zingine kwenye uteuzi huo.
Kulingana na mwenyekiti wa jamii ya Somik na masai elgon Francis Chemwor hatua ya kutowasilishwa kwa majina kutoka pande zote na kutohusishwa kwa jamii zote huenda ikaibua mgawanyiko baina ya jamii hizo wakati wa uchaguzi mkuu.
Chemwor aidha amesema ili kuwe na amani, umoja na maendeleo katika jamii pana haja ya maoni ya viongozi wote kutoka jamii husika kuskizwa.