JAMII YA POKOT INAYOISHI NCHINI UGANDA IMEMSIFIA RAIS YOWERI MUSEVENI KWA KUFANIKISHA AMANI MIONGONI MWAO

Huku uchaguzi mkuu wa taifa la Uganda ukiwa umekaribia kufanyika, wakazi wa jamii ya Pokot wanaoishi katika Eneobunge la Amudat nchini humo, wamemsifia Rais wa sasa Yoweri Kaguta Museveni kwa kufanikisha kuwapo kwa amani baina ya jamii hiyo na jamii ya Karamoja.

Wakiongozwa na mmoja wa wakazi hao Daniel Tiyan wamesema kwa ushirikiano na mbunge wao Christopher Domo, Rais Museveni amefanikisha pia maendeleo mengi ambapo anafaa kupigiwa kura mara nyingine ili aweze kudumisha amani hiyo pamoja na kutekeleza maendeleo mengine.

Wakati uo huo Tiyan amemsifia Christopher kwa kutuliza joto la wizi wa mifugo baina ya jamii za Sebei, Karamoja na jamii ya Pokot akiwa anashirikiana na Museveni kwenye Chama cha National Resistance Movement NRM.