JAMII YA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI NI JAMII SALAMA


Dunia inafaa kubadili mtazamo wao kuhusu kaunti hii ya pokot magharibi.
Haya ni kwa mujibu wa mwakilishi kina mama kaunti Hii Lilian Tomitom ambaye amesema kuwa ni watu wachache tu ambao wanendeleza uhalifu wa wizi wa mifugo wala si jamii nzima hivyo haifai kuonekana kuwa jamii isiyo salama.
Aidha Tomitom ametumia fursa hiyo na kusema kuwa matokeo bora ambayo kaunti hii imeandikisha kwenye matokeo ya mtihani wa taifa kwa darasa la nane KCPE yanafaa kuwa ujumbe halisi kwa taifa kuwa jamii hii inatilia maanani umuhimu wa masomo wala si wizi wa mifugo.