JAMII TRANS NZOIA YAHIMIZWA KUTUNZA MISITU.


Zaidi ya washikadau 300 kutoka sekta ya utalii na mazingira wameshiriki matembezi ya kilomita 7 katika mbuga ya kitaifa ya Saiwa ili kuhamasisha kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira ili kuzuia kupotea kwa swara aina ya sitatunga katika mbunga hiyo ya Wanyama eneo bunge la Cherangani Kaunti ya Trans-Nzoia.
Wakiongozwa na mkurugenzi wa mbuga za Wanyama eneo la Magharibi mwa Kenya Catherine Wambani amesihi umma kuzingatia utunzaji wa msitu na chemichemi iliyoko kwenye mbuga hiyo ya wanyama ili kuhakikisha Sitatunga na wanyama wengine mbugani humo wanalindwa na kuhifadhiwa.
Kwa upande wake Mwanzilishi wa mradi wa Nyumbani Kwetu Paul Kurgat ameghadhishwa na wizara ya utalii kwa kukosa kutilia maanani sekta ya Utalii Kaunti ya Trans-Nzoia jambo ambalo limepelekea sekta hiyo kudidimia.