IEBC YAPONGEZWA KWA KUSHINIKIZA THULUTHI MBILI YA JINSIA YA WAGOMBEA KATIKA VYAMA VYA KISIASA.


Viongozi wa kike katika kaunti ya Trans nzoia wameipongeza tume ya uchaguzi na mipaka IEBC kwa kuvishinikiza vyama vya kisiasa kuwasilisha orodha ya wagombea wao ambayo inaafiki thuluthi mbili ya uwakilishi wa jinsia.
Wakiongozwa na Catherine Nanjala, viongozi hao wamesema kuwa vyama mbali mbali vya kisiasa nchini vilikuwa vikiwakandamiza wanawake hali ambayo imehujumu pakubwa azma za wanawake wengi kugombea viti vya uongozi na kulemaza juhudi za kuafikia hitaji la kikatiba la thuluthi mbili ya uwakilishi wa jinsia katika uongozi nchini.
Viongozi hao wamesema kuwa inasikitisha kuona kuwa katika karne ya sasa wanawake bado wanakandamizwa katika maswala ya uongozi nchini kwa kutopewa nafasi sawa na wanaume, swala wanalosema kuwa huenda likaathiri vizazi vijavyo.