IEBC YAENDELEA KUIDHINISHA WAGOMBEA NYADHIFA ZA KISIASA AGOSTI 9.


Wagombea nyadhifa mbali mbali katika kaunti hii ya Pokot magharibi wameidhinishwa rasmi na tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kuwania nyadhifa hizo katika uchaguzi mkuu wa tarehe tisa mwezi agosti mwaka huu.
Miongoni mwa waliodihinishwa ni pamoja na mbunge wa Kapenguria Samwel Moroto na mgombea ubunge wa Pokot Kusini James Teko.
Wakizungumza baada ya kuidhinishwa rasmi, wawili hao wameelezea kuridhishwa na mchakato huo wakisema hatua ya kuidhinishwa kwao sasa inatoa fursa kwao kuendesha kampeni ikizingatiwa sasa kipindi cha kampeni kimeanza rasmi.
Aidha viongozi hao wamesisitiza haja ya kudumishwa amani miongoni mwa wananchi pamoja na wanasiasa kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi mkuu ili kuwe na utilivu nchini kabla, wakati na hata baada ya uchaguzi huo wa agosti 9.