IDARA ZA USALAMA ZATAKIWA KUCHUNGUZA MADAI YA KUFURUSHWA MTOTO CHELOMBEI


Wito umetolewa kwa idara husika katika kaunti hii ya Pokot magharibi kuchukulia hatua jamii moja eneo la Chelombey Kacheliba kwa kumfurusha mtoto mwenye umri wa miaka 11 na kumlazimu kutembea kutoka eneo hilo hadi mjini Makutano.
Wahudumu wa boda boda mjini Makutano ambao wamempata mtoto huyo kwa jina Bonface Ruto wameelezea ghadhabu zao hasa ikizingatiwa mtoto huyo alifaa kutembea hadi eneo la Kanyarkwat waliko wazazi wake.
Wahudumu hao sasa wanatoa wito kwa wazazi kaunti hii kuwatunza wanao wenyewe na kutowaweka chini ya ulinzi wa watu wasio wa jamii yake ili kuzuia visa kama hivi kutokea.
Kwa upande wake mhusika ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi ya Chelombei amesema kuwa alifurushwa na mwenyeji wake bila kupewa nauli ya kumwezesha kufika nyumbani.