IDARA YA USALAMA POKOT MAGHARIBI YATAKIWA KUIMARISHA USALAMA WA SEKTA YA BODA BODA.


Wito umetolewa kwa sekta ya boda boda hasa maeneo ya Chepareria na Kacheliba kaunti hii ya Pokot magharibi kuwa na mipangilio madhubuti ambayo itazuia mianya ya wezi wa pikipiki kuendeleza uovu huo.
Ni wito wake mwenyekiti wa wahudumu wa boda boda katika kaunti ndogo ya Kapenguria Laban Ruto ambaye aidha ametoa wito kwa idara ya usalama kushirikiana na sekta hiyo ili kuhakikisha kuwa visa hivi ambavyo vimekithiri kaunti hii vinashughulikiwa ipasavyo.
Aidha ruto amewaonya wazazi katika kaunti hii dhidi ya kuwaruhusu wanao wenye chini ya umri wa miaka 18 kuendesha pikipiki akionya kuwa hatua zitachukuliwa dhidi ya wahusika kauli ambayo imetiliwa mkazo na naibu mwenyekiti wa wahudumu hao moses kemoi.
Aidha viuongozi hao wametoa wito kwa wahudumu wa boda boda kutokubali kutumika visivyo na wanasiasa hasa wakati huu ambapo siasa za uchaguzi mkuu wa mwezi agosti zimeshika kasi na badala yake kuzingatia shughuli zao na kuwachagua viongozi bora utakapowadia wakati wa uchaguzi.