IDARA YA USAJILI WA WATU YATAKIWA KUHARAKISHA UTOAJI VITAMBULISHO KWA WAKAZI TRANS NZOIA.


Viongozi wa kisiasa nchini wameendelea kushinikiza kuharakishwa utoaji wa vitambulisho kwa wenyeji hasa waliotimu umri wa kujisajili kuwa wapiga kura.
Wakiongozwa na mbunge wa kwanza kaunti ya Trans nzoia Ferdnand wanyonyi pamoja na agostino neto viongozi hao wamesema kuwa wengi wa wakenya hasa akina mama kutoka maeneo ya mipakani hawana stakabadhi hizo kufuatia ugumu wa kuzipata.
Aidha wabunge hao wamelalamikia kile wamedai baadhi ya wakenya wanasafirishwa kutoka maeneo mengine na kujisajili ili kupigia kura maeneo tofauti, wakiwataka wakenya kutokubali mbinu hizo za baadhi ya wanasiasa kwani hazikubaliki kisheria na kamwe hazitofaulu.