IDARA YA POLISI POKOT MAGHARIBI YAHUSISHWA KATIKA UPANZI WA MITI.
Wito umetolewa kwa vijana katika kaunti hii ya Pokot magharibi kujitenga na maswala ya uhalifu na badala yake kujihusisha na shughuli zitakazowapelekea kupata riziki zao za kila siku.
Akizungumza baada ya kupokea miche alfu 3,500 kutoka kwa kikundi cha mtelo global warming network, kamanda wa polisi kaunti hii Peter Katam amepongeza kuhusishwa idara ya polisi katika shughuli ya upanzi wa miti anayosema ni muhimu zaidi katika kuhifadhi mandhari ya vituo vya polisi kaunti hii.
Aidha katam amepongeza kundi hilo la vijana kwa kuendeleza shughuli ya upanzi wa miti akitoa wito kwa vijana zaidi kaunti hii kujihusisha na shughuli hiyo anayosema kuwa itasaidia katika kukabili visa vya vijana kujihusisha na visa vya uhalifu ikiwemo wizi wa mifugo.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na mwenyekiti wa kikundi hicho Benson Pilipili ambaye pia amesema wanashirikiana na maafisa wa polisi katika shughuli hiyo katika kuwahamasisha vijana kuhusu umuhimu wa kujihusisha na shughuli za kuwanufaisha maishani.