IDARA YA MEGEREZA KWENYE KAUNTI BUNGOMA INAKUBWA NA HOFU YA MSAMBAO WA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA CORONA KUFUATIA UHABA WA MAJI


Idara ya magereza kwenye kaunti ya Bungoma ni mojawapo ya idara ambazo zinaendlea kuathirika pakubwa kutokana na ukosefu wa maji waki huu wa janga la corona.
Msimamizi wa gereza hilo Hassan Mkabani amesema kwamba gereza hilo lenye zaidi ya wafungwa 800 linakabilwa na ukosefu wa maji hali inayosambaratisha mazingira bora kwa wafungwa.
Mkabana aidha anahofia kwamba huenda hali hiyo ikachangia pakubwa kusambaa kwa virusi vya corona ikizingatiwa kwamba tayari kuna wafungwa saba na wafanyakazi watatu ambao wamethibitishwa kuwa na virusi vya corona