IDARA MBALIMBALI KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI YAKAMILISHA KIKAO CHA KWANZA CHA MAKADIRIO YA BAJETI.


Kikao cha Kamati ya makadirio ya bajeti ya kaunti ya Pokot Magharibi imewahusisha maafisa wa idara mbalimbali katika kaunti hii pamoja na wakazi wachache ilikamilika vyema katika ukumbi wa maonyesho ya kilimo ya Kishaunet.
Akizungumza na kituo hiki cha kalya radio , waziri wa kilimo na mifugo Geoffrey Lipale amesema idara yake imewasilisha maombi kadhaa katika wizara ya fedha huku akiweka kipaumbele miradi ya unyunyuziaji maji mashamba, na usambazaji wa mbegu za kitunguu pamoja na mimea nyingine.

Ameongeza kwamba mradi wa ukuzaji wa mbegu wa mifugo maarufu Nasukuta unapaniwa kupanuliwa na kujengwa kwenye maeneobunge yote katika gatuzi la Pokot Magharibi ili tatizo la usafirishaji wa mbegu hizo kutoka magatuzi mengine liweze kutatuliwa.
Afisa mkuu katika wizara ya fedha Milcah Siwa kwa upande wake amesema mkutano huo umekuwa wa awamu ya kwanza ya makadirio ya bajeti huku mikutano mingine ya kuwahusisha raia kikamilifu ikitarajiwa kufanyika kwenye wadi zote katika kaunti hii.
Siwa ameongeza kwamba serikali ya kaunti hii inapania kuikamilisha miradi ambayo tayari ilikuwa imeahidiwa ikiwamo kiwanda cha maziwa katika eneo la Lelan na kiwanda cha matunda ambacho kinatarajiwa kuanzishwa mjini Ortum pamoja na miradi mingine muhimu.
Mwenyekiti wa bajeti katika kaunti ya pokot maghaibi na ambaye pia ni mwakilishi wa wadi ya tapach korinyang timtim alimesema kwamba serkali ya kaunti ya pokot magharibi inapata kiwango kidogo cha mgao wa kaunti kutokana ukusanyaji mdogo wa ushuru kaunti hii.

[wp_radio_player]