IDADI YA WASICHANA AMBAO WAMEREJELEA MASOMO YAO KAUNTI HII YA POKOT MAGHARIBI NI YA CHINI

Waziri wa elimu katika kaunti ya Pokot Magharibi Ruth Kisabit ametaja mimba za mapema na kuwaoza wasichana mapema katika kaunti hii kuwa kigezo kikuu cha kushuhudia idadi ndogo ya wasichana ambao wameripoti shuleni hadi sasa.

Kisabit amesema wapo wasichana ambao wamejifungua tayari na wamerejea shuleni kuendelea na masomo yao japo wengi wao hawajaripoti shuleni kwa kukosa wale ambao watashughulikia malezi ya wanao.

Akizungumza na wanahabari Kisabit hata hivyo amesema watoto wachanga nao wana haki ya kunyonyeshwa na mama zao hadi watakapokomaa ili kuepuka magonjwa yanayotokana na ukosefu wa lishe bora.

Kisabit hata hivyo amewahimiza wazazi kwa ushirikiano na walimu kuchukua suala la wanafunzi wanaonyonyesha kwa uzito ili waweze kuhakikisha wanasoma wakiwatunza wanao nyumbani.