IDADI YA WANAFUNZI WANAOHUDHURIA MASOMO YAPUNGUA CHERANG’AN POKOT MAGHARIBI.

Na Dismas Terer.

Idadi ya wanafunzi wanaohudhuria masomo hasa katika shule za msingi eneo la cherang’an katika wadi ya Kodich kaunti hii ya Pokot magharibi imepungua pakubwa kutokana na kukithiri baa la njaa miongoni mwa familia nyingi eneo hilo.
Akizungumza baada ya shughuli ya kukagua hali ya wanafunzi kuhudhuria masomo katika shule mbali mbali iliyoongozwa na kamati inayohusisha idara ya usalama na elimu eneo hilo, mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Cherang’an Benjamin Kiprop ameitaka serikali kuangazia swala la chakula shuleni ili kuwawezesha wanafunzi kuhudhuria masomo.
Wakati uo huo Kiprop ametoa wito kwa serikali ya kaunti kuendeleza mpango wa kutoa uji kwa wanafunzi wa shule za chekechea hadi katika shule za msingi.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na chifu wa eneo la Cherang’an Benjamin Atelatum ambaye amesema licha ya baadhi ya shule kufadhiliwa na shirika la umoja wa matiafa linashughulikia watoto UNICEF kwa maswala ya chakula, lipo hitaji kubwa la chakula shuleni ili kufanikisha shughuli za masomo.