IDADI YA VYOO KASEI YATAJWA KUWA YA CHINI MNO.
Idadi kubwa ya jamii katika eneo la Kasei kaunti hii ya Pokot magharibi hazina vyoo.
Haya ni kulingana na afisa wa afya ya umma eneo hilo Richard Chepkwony ambaye amesema kuwa ni kati ya asilimia 7 hadi kumi pekee ya familia ambazo zina vyoo eneo hilo hali ambayo inachangia ongezeko la magonjwa yanayotokana na uchafu.
Chepkwony amesema licha ya kuwa yapo baadhi ya mashirika ya kijamii ambayo yanasaidia katika kuwahamasisha umma kuhusu umuhimu wa ujenzi wa vyoo, wengi wa wakazi eneo hilo bado hawajakumbatia swala hilo.