IDADI NDOGO YA VIJANA KUTOKA KAUNTI YA TRANS NZOIA INAJIUNGA NA VYUO VYA KIUFUNDI


Serikali ya Kaunti ya Trans-Nzoia kupitia kwa wizara ya Elimu ya kiufundi imelalamikia idadi ndogo ya wanafunzi wanaojiunga na vyuo vya anwai licha ya serikali ya kaunti kuekeza pakubwa katika vyuo hivyo mbali na idadi kubwa ya wanafunzi kukosa nafasi katika vyuo vikuu nchini.
Akihutubu katika wadi ya Kiminini wakati wa warsha ya kuhamasha vijana kuhusu umuhimu wa kupata Elimu ya kiufundi, Eliud Lusweti mkurugenzi wa Elimu ya kiufundi Kaunti ya Trans-Nzoia amelaumu dhana kuwa vyuo vya anwai ni vya wafunzi waliofeli mtihani, akitoa wito kwa vijana kujiunga na vyuo hivyo kwani serikali ya kaunti inatoa ufadhili wa vifaa vya kiufundi baada ya mwanafunzi kufuzu.
Kwa upande wake mwakilishi wadi ya Kiminini David Kisaka amewarai viongozi wengine kuekeza zaidi katika Elimu ya kiufundi kupitia kwa vyuo hivyo, akisisitiza haja ya vijana kujihususha na maswala ya kilimo.
Mshirirkishi wa mradi wa Simama Kiminini Emmanuel Masika amesema kupitia kwa Elimu ya kiufundi vijana wengi watapata nafasi ya kupata ujuzi na kujiajiri wenyewe hivyo kukabili ukosefu wa ajira na visa vya utovu wa midhamu miongoni mwa vijana ikiwa na pamoja na matumizi ya miadharati.