HUENDA WANAFUNZI KUTOKA ENEOBUNGE LA BARINGO KUSINI WAKAKOSA KUREJEA SHULENI


Huku shule zikifunguliwa leo hii, huenda wanafunzi wanaosomea katika shule zilizoko eneo la Arabal, Chemorongion na Kapindasum eneo bunge la Baringo Kusini Kaunti ya Baringo wakakosa kufungua shule kufuatia utovu wa usalama ambao umechangiwa na visa vya uvamizi na wizi wa mifugo eneo hilo.
Kulingana na mbunge eneo hilo Charles Kamuren ni kwamba wakazi wameanza kuhama makwao kutokana ma kudorora kwa usalama ambapo ameitaka serikali kuingilia kati na kuhakikisha usalama unaimarishwa ili kuwawezesha wanafunzi kurejea shuleni.
Kamuren aidha ametilia shaka oparesheni ya kutwaa silaha haramu inayoendelezwa eneo hilo akisema kuwa huwenda serikali inahadaa kuwa msako unaendela ilhali hakuna lolote linalofanyika kufuatia kuongezeka visa vya uvamizi.
Wakazi kwa upande wao wamesema kuwa kwa sasa wanaishi kwa hofu na kwamba hawatawaruhusu wanao kwenda shuleni iwapo serikali haitawahakikishia usalama wao.