HUENDA MASAIBU YA WALIMU WA KNUT YAKAFIKA KIKOMO KARIBUNI.


Katibu mkuu wa chama cha walimu nchini knut tawi la kaunti ya trans nzoia George Wanjala ameelezea matumani kuwa maslahi ya walimu yatashughulikiwa hasa baada ya uhusiano bora kuanza kushuhudiwa baina ya chama hicho na mwajiri wao TSC.
Aidha wanjala ameiomba TSC kuyarejesha majina ya wanachama ambayo yaliondolewa katika sajili ya KNUT.
Kwa upande wake mwenyekiti wa KNUT katika kaunti ya Trans nzoia Wilberforce Wamalwa ameirai wizara ya afya kuweka mikakati ya kuwapa walimu chanjo dhidi ya virusi vya corona ili kuhakikisha usalama wa walimu hao.
Ikumbukwe bunge la kitaifa liliagiza TSC mwaka uliopita kuyarejesha majina ya walimu alfu 130 katika sajili ya KNUT baada ya kuyaondoa.