HUDUMA ZA MAZISHI ZAPIGWA MARUFUKU KARIBU NA HOSPITALI KAUNTI YA TRANS NZOIA.


Gavana wa Kaunti ya Trans-Nzoia Patrick Khaemba ametoa agizo la kupiga marufuku biashara ya huduma za mazishi na kuondolewa Mara moja karibu au kwenye barabara kuu za kuelekea hospitalini katika Kaunti hiyo.
Akihutubu mjini Kitale Khaemba amesema licha ya huduma hiyo kuwa muhimu ipo haja ya kutafuta mahala mwafaka pa kuweka na kutangaza huduma hiyo akisema hatua hiyo inawakera wengi haswa wanaotafuta huduma za afya katika hospitali hizo.
Aidha Khaemba amesema tayari notisi ya kuondolewa kwa bishara hizo imetolewa na serikali yake akisema wanaotoa huduma hizo hawakufuata sheria na kanuni za kuweka bishara hizo akisisitiza watakaokiuka agizo hilo wataondolewa kwa nguvu.