HOSPITALI YA ST RAPHAEL MATISI YANUFAIKA NA SHILINGI MILIONI 4.1


Siku chache baada ya mbunge wa Saboti Caleb Amisi kuwasilisha mswada kwa kamati ya Afya katika bunge la Kitaifa kutaka bima ya afya ya Kitaifa NHIF kulipa Hospitali ya St Raphael iliyoko kwenye mtaa wa matisi deni la shilingi M4.1 sasa bima hiyo imetoa fedha hizo.
Kwenye mkao na wanahabri mjini Kitale Amisi amesema ni afuaeni kuu kwa Hospitali hiyo kwani fedha hizo zitasaidia katika upanuzi wa Hopspitali hiyo mbali na kuimarisha huduma kwa wenyeji wa mtaa huo.
Wakati huo huo Amisi amepongeza hatua ya mkewe rais Bi Margaret Kenyatta kwa kuanzisha mpango wa huduma ya afya kwa akina Mama kwa jina linda Mama ambao amesema umepiga jeki pakubwa utoaji wa huduma ya kujifungua kwa akina Mama haswa kwenye maeneo ya mabanda, ikikimbukwa kwamba Kaunti ya Trans-Nzoia imeandikisha idadi kubwa ya mimba za mapama miongoni mwawanafunzi.