HOSPITALI YA RUFAA YA LODWAR HAINA VIFAA VYA KUTOSHA VYA KUWASHUGHULIKIA WAGONJWA


Baadhi ya viongozi kwenye kaunti ya Turkana wamekashfu vikali utepetevu katika hospitali ya rufaa ya Lodwar wakisema hospitali hiyo haina vifaa vya kutosha kuwahudumia wagonjwa mahututi.
Hali hiyo imewalazimu wagonjwa kupelekwa kwenye hospitali ya rufaa ya Eldoret licha ya hospitali ya Lodwar kupewa kiwango cha rufaa pamoja na madaktari waliofuzu kwenye nyanja mbalimbali.
Haya yanajiri baada ya visa vya wizi wa dawa na watu kufariki dunia kila mara kuripotiwa katika taasis hiyo huku wengine wakiishtaki kwa kuwapoteza wapendwa wao kwa njia ya kutatanisha.
Mbunge wa Turkana ya kati John Lodepe amesema kwamba wakaazi wa Turkana wanagharamika hata zaidi kuwasafirisha wapendwa wao kuenda kuhudumiwa Eldoret.
Kwa upande wake mbunge mwa Loima Jeremiah Lomorkai amemuhimiza waziri wa afya wa kaunti Jane Ajele kuwajibikia swala hilo kwa kulinda masilahi ya madaktari na kuwapa marupurupu ya kutosha.