HOSPITALI YA KAPENGURIA YAPOKEA VIFAA VYA MATIBABU KUTOKA KEMSA.

Na Benson Aswani

Serikali ya kaunti ya Pokot magharibi imepigwa jeki katika shughuli za kutoa huduma za kiafya baada ya kupokea vifaa vya matibabu pamoja na dawa kutoka mamlaka ya kusambaza dawa na vifaa vya matibabu nchini KEMSA.
Miongoni mwa vifaa ambavyo vimepokezwa hospitali ya kapenguria ni pamoja na glavu na dawa za kukabili makali ya virusi vya HIV, ARVs.
mwanafamasia wa hospitali ya Kapenguria Musa Kibet amesema kuwa vifaa hivyo vitasambazwa katika vituo vyote 94 vya afya katika maeneo mbali mbali ya kaunti hii ya Pokot magharibi.