HOSPITALI YA KACHELIBA YAKANUSHA MADAI YA UHABA WA DAWA.
Siku chache tu baada ya wakazi kutoka eneo la kacheliba kaunti hii ya pokot magharibi kulalamikia huduma duni katika hospitali ya kacheliba kufuatia uhaba wa dawa, uongozi wa hospitali hiyo umewahakikishia wakazi uwepo wa huduma bora.
Msimamizi wa hospitali hiyo Solomon Tukei amesema kuwa japo vipo vifaa mbali mbali vya matibabu ambavyo bado havijafika, hospitali hiyo kwa sasa ina dawa za kutosheleza mahitaji ya wakazi kwa sasa wakati ambapo vifaa vingine vya matibabu vinatarajiwa.
Tukei amewataka wakazi kutoiharibia sifa hospitali hiyo kwa kueneza madai ya kutokuwepo dawa akisema kuwa ukosefu wa dawa ambayo mgonjwa mmoja anaitisha hakumaanishi kuwa sasa dawa zote hazipo, akikariri kuwa uongozi wa hospitali hiyo unajitahidi kuhakikisha huduma bora.
Wakati huo Tukei ametoa wito kwa wagonjwa wanofika katika hospitali hiyo kutafuta huduma mbali mbali ikiwemo kupimwa sampuli za damu kulipia huduma hizo kwani ni kupitia fedha hizo ambapo baadhi ya vifaa hununuliwa.