HOFU YA UPUNGUFU WA CHAKULA YATANDA TRANS NZOIA.


Viongozi Kaunti ya Trans Nzoia wameelezea hofu ya kupungua kwa uzalishaji wa zao la mahindi mwaka huu kwa zaidi ya asilimia hamsini.
Wakiongozwa na Naibu Gavana Kaunti ya Trans Nzoia Dkt Stanley Tarus viongozi hao wamesema hii ni kutokana na uvamizi wa viwavi jeshi pamoja na kiangazi ambacho kilishuhudiwa mwanzoni mwa mwaka huu kote nchini.
Aidha Tarus ametoa changamoto kwa wakulima kanda hii kukumbatia kilimo mseto kama njia Moja ya kukabiliana na magonjwa na wadudu ibuka pamoja na mabadiliko ya hali ya anga nchini, akisema ni kupitia kwa njia hiyo pekee ndipo mkulima ataweza kuepuka hasara.