HITAJI LA SHAHADA KWA WANAOWANIA NYADHIFA ZA SIASA LAENDELEA KUPINGWA.


Viongozi katika kaunti ya Trans nzoia wameendelea kupinga hitaji la wanaolenga kuwania nyadhifa za kisiasa nchini kuwa na shahada.
Mgombea kiti cha ubunge eneo bunge la Cherangíani John Njuguna amesema kuwa sheria hiyo ni mbinu moja ya kuwazuia baadhi ya viongozi ambao wametangaza nia ya kugombea nyadhifa za uongozi katika uchaguzi mkuu ujao.
Akiunga mkono juhudi za walioelekea mahakamani kupingi hitaji hilo Njuguna ameitaka mahakama kufutilia mbali sheria hiyo anayosema kuwa itawanyima haki wakenya wengi kuwachagua viongozi wanaowapendelea kwa misingi ya kutokuwa na shahada.