HITAJI LA KUWA NA SHAHADA KWA WANAOWANIA NYADHIFA ZA SIASA LAENDELEA KUZUA HISIA.


Hisia mbalimbali zinazidi kutolewa kuhusiana na hitaji la wanaotaka kuwania viti mbalimbali kuwa na shahada.
Mwakilishi wadi wa Matumbei eneo bunge la Endebes kaunti ya Trans nzoia Jeremiah Wakhulia amesema iwapo sheria hiyo haitabadilishwa itawalazimu viongozi hao kutafuta vyeti hivyo la asivyo watakosa nafasi hizo.
Aidha wakhulia amepuuzilia mbali dhana kuwa kiongozi ni mwanasiasa pekee akisema mtu anaweza kuwa kiongozi katika nyanja mbalimbali, akitoa wito kwa tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kulegeza kamba na kuwaruhusu viongozi walioonyesha nia ya kupata vyeti hivyo kuwania nyadhifa hizo.

[wp_radio_player]