HISIA ZINAENDELEA KUTOLEWA KUHUSIANA NA JOPO LILILOBUNIWA LA KUANGAZIA MTAALA WA CBC POKOT MAGHARIBI.

Viongozi wa miungano ya walimu maeneo mbali mbali ya nchi wameendelea kuibua hisia mbali mbali kuhusiana na hatua ya rais William Ruto kubuni jopo la kuangazia utekelezwaji wa mtaala mpya wa elimu CBC.

Wa hivi punde kutolea hisia hatua hiyo ni katibu mkuu wa chama cha walimu nchini KNUT tawi la Pokot magharibi Martine Sembelo ambaye amesema kuwa jopo hilo lingewajumuisha zaidi wadau katika sekta ya elimu hasa vyama vya walimu kwani ndio wanaofahamu zaidi changamoto ambazo zinatokana na mtaala huo.

Sembelo amesema kwamba iwapo mchakato mzima wa utekelezwaji wa mtaala huu hautawahusisha wadau wanaohusika moja kwa moja hasa walimu na wazazi huenda ukakosa kuafikia malengo hitajika.

Wakati uo huo Sembelo ametoa wito kwa wakuu wa shule katika kaunti hii kuelewana na wazazi kuhusu jinsi ya kulipa karo na kutowatuma wanafunzi nyumbani akisema kuwa wakati huu ni mgumu zaidi kiuchumi kwa wazazi, na kwamba muhula huu ni mfupi zaidi kwa wanafunzi kupotezea muda mwingi barabarani.

[wp_radio_player]