HISIA ZA IBULIWA KUHUSIANA NA CHAMA KIPYA POKOT


Uanzilishi wa Chama cha Kenya Union Party KUP katika Kaunti hii ya Pokot Magharibi umeibua hisia mbalimbali miongoni mwa wakazi wa kaunti hii.
Kulingana na Mzee Gabriel Lonyiko mkazi wa Kacheliba, Chama hicho kimeanzishwa wakati ambapo tayari vyama vingine vimejipanga katika uchaguzi mkuu ujao.
Aidha Lonyiko amesema chama hicho hakijawajumuisha viongozi wa kaunti hii hali ambayo amesema itasababisha mgawanyiko zaidi miongoni mwa viongozi.
Kwa upande wake Joseph Sarich amekishabikia Chama hicho akitaja kwamba ni mwanga mpya kwa wakazi wa kaunti ya Pokot Magharibi kwa sababu kitatoa nafasi nzuri ya mazungumzo baina ya jamii ya Pokot na meza ya kitaifa.