HISIA ZA ENDELEA KUTOLEWA BAADA YA KUAPISHWA KWA GAVANA SIMON KACHAPIN KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI


Viongozi mbali mbali wa kaunti hii ya Pokot magharibi wameendelea kupongeza kuapishwa rasmi gavana wa kaunti hii Simon Kachapin kuanza tena kuhudumu kama gavana wa kaunti hii.
Wakiongozwa na mbunge wa Kacheliba Mark Lumnokol, mwenzake wa Sigor Peter Lochakapong na Samwel Moroto wa Kapenguria, viongozi hao wamesema kwamba kaunti hii imepata chaguo bora la kiongozi wakielezea imani kwamba kaunti hii itaafikia viwango vya maendeleo ambavyo vinahitajika chini ya gavana Kachapin.
Wamesema kuwa wataendelea kushirikiana na Kachapin katika muhula wake wa utendakazi kwa manufaa ya mkazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi.
Ni kauli ambayo imetiliwa mkazo na mbunge wa Kapenguria Samwel Moroto ambaye aidha amepongeza hali ya utulivu ambayo imeshuhudiwa katika hafla hiyo licha ya tofauti za kisiasa, akiwataka wakazi wa kaunti hii kuendelea kushirikiana ili kuwe na umoja miongoni mwao.