HISIA KUHUSU MSWADA WA MAREKEBISHO YA KATIBA WA 2020 ZAENDELEA KUTOLEWA NA WAKAAZI WA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI
Huku kamati maalum iliyobuniwa kuongoza mchakato wa kufanyia katiba marekebisho kupitia BBI ikitangaza kujiandaa kuipigia debe BBI kote nchini baada ya mabunge ya kaunti kuidhinisha mswada huo, wakaazi wa kaunti ya pokot magharibi wametoa hisia zao kuhusu mswada huo na endapo wako tayari kwa kura ya maoni.
Wakaazi hao wameelezea hisia kinzani kuhusu BBI huku wanaopinga wakisema hawakotayari kushiriki kura ya maoni.
Nao wanaoshabikia mpango huo wa BBI wamesema hawatakubali tena kupotoshwa na viongozi kuhusu katiba kama ilivyofanyika wakti wa kuipitisha katiba ya 2010.
Licha ya kuwepo tofauti za hisia , wakaazi hao hata hivyo wanawashauri wakenya kutogawanywa kwa misingi ya kisiasa na kikabila wanaposhiriki kwenye maswala ya kisiasa. Haya yanajiri baada huku bunge la kaunti ya pokot magharibi Likiwa miongoni mwa mabunge yaliyoidhinisha mswada huo wa marekebisho ya katiba.