HISIA KALI ZAENDELEA KUFUATIA UHABA WA UNGA WA BEI NAFUU.


Mwakilishi kina mama kaunti ya Trans nzoia Janet Nangabo amemtaka waziri wa kilimo Peter Munya kuingilia kati na kuhakikisha unga wa bei nafuu uliotangazwa na serikali  unapatikana madukani ili
kuhakikisha  wakazi hawakandamizwi na wafanyibiashara wanaoendelea kuwauzia bidhaa hiyo kwa  bei ghali.

kauli ya Nangabo inajiri baada ya wakazi kulalamika kuhusiana masharti makali yanayowataka wanunue  pakiti mbili za unga pekee wakitaka serikali kuhakikisha unga huo unafika maeneo ya mashinani.
Nangabo amemuomba waziri munya kuhakikisha unga huo unapatikana maeneo yote nchini na pia wananchi wanauziwa kwa bei iliyotangazwa na serikali.
wakati uo huo Nangabo amewataka wakazi wa kaunti hiyo ya Trans nzoia kujiepusha na siasa za  kutumiwa vibaya kuzua vurugu kwenye mikutano ya hadhara haswa wakati huu zikiwa zimesalia siku saba pekee kabla ya uchaguzi wa mwezi agosti.