HAZINA YA TAIFA YATAKIWA KUAHARAKISHA KUTOA FEDHA KWA IEBC.

Na Benson Aswani
Mbunge wa Kapenguria Samwel Moroto ameitaka hazina ya taifa kuharakisha katika kutoa fedha kwa tume ya uchaguzi na mipaka IEBC ili kuiwezesha kufanikisha shughuli ya usajili wa wapiga kura wapya baada ya agizo la mahakama la kuitaka kuendeleza zoezi hilo kwa siku zingine 7.
Moroto amesema kuwa tume hiyo ilitengewa mgao finyu wa kuendesha zoezi hilo hali iliyoifanya kusitisha zoezi hilo jumanne wiki hii hali iliyowalazimu kuishinikiza serikali kuongeza fedha hizo ili kuwezesha usajili wa wapiga kura zaidi.
Wakati uo huo Moroto ametaka idara ya usajili wa watu kurahisisha shughuli ya utoaji wa vitambulisho ili kuwapa fursa vijana kujisajili na kuwa katika nafasi bora ya kuwachagua viongozi wanaowapendelea katika uchaguzi mkiuu wa mwaka ujao.