‘HATUNA HOFU NA USALAMA WA CHAKULA POKOT MAGHARIBI’ YASEMA NDMA.


Mamlaka ya kushughulikia majanga NDMA kuanti hii ya pokot magharibi imeendeleza vikao vya kuangazia hali ya chakula katika kaunti hii ya pokot magharibi na kubaini maeneo ambayo yatahitaji misaada kutokana na ukame uliopelekea kuathirika mimea ya wakulima wengi mwanzoni mwa mwaka huu.
Akizungumza baada ya kikao hicho ambacho pia kilinuia kuweka mikakati ya kukabili majanga katika kaunti hii naibu mkurugenzi wa habari kuhusu ukame katika mamlaka hiyo Joshua Mayeku amesema kuwa ikizingatiwa wakulima katika kaunti hii wanategemea zaidi mifugo, idadi kubwa ya wakazi hawataathirika zaidi kutokana na hali ya ukame.
Japo amekiri mavuno ya wakulima yatapungua pakubwa mwaka huu, amesema kuwa hali haijakuwa mbaya zaidi ilivyokuwa ikikadiriwa kwani mvua ya msimu ambayo imekuwa ikishuhudiwa katika kaunti hii imepelekea uwepo wa chakula cha mifugo hali ambayo ni afueni kwa wakazi.
Hata hivyo amesema kuwa maeneo ya mipakani mwa kaunti hii ya pokot magharibi na kaunti jirani ikiwemo Elgeyo marakwet, Baringo na Turkana ndiyo yanayofaa kutazamwa zaidi kutokana na utovu wa usalama ambao uekuwa ukishuhudiwa maeneo hayo.