HATUA YA SERIKALI KUFUNGA MAENEO YA IBADA KATIKA KAUNTI 13 YAENDELEA KUKASHIFIWA VIKALI


Hatua ya serikali kufunga kaunti 13 za eneo la Magharibi, Nyanza na Bonde la ufa kutokana na idadi ya maambukizi ya virusi vya corona imeendelea kukashifiwa vikali.
Viongozi wa kidini kaunti ya Trans Nzoia kasisi wa kanisa la Elim Pentecoastal Kenya Bonfase Oduor amesema kuwa serikali haikustahili kufunga maeneo ya ibada kwani sheria zote za kuzuia maambukizi zilikua zinafuatwa.
Akizungumza mjini KItale kasisi Oduor amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kwa serikali kufunga maeneo ya ibada ilhali vyumba vya burudani vinaendelea na shughuli zake hadi siku ya jumapili.
Oduor ameirai serikali kulegeza masharti hayo na kuruhusu hafla za ibada kurejelewa akisema kwamba kama viongozi watahakikisha waumini wate wanaofika kwenye maeneo ya ibada wanafuata masharti ya kukabili korona.