HATUA YA MUDAVADI KUSHIRIKIANA NA RUTO YAZIDI KUIBUA HISIA NCHINI.
Hisia mseto zimeendelea kuibuliwa nchini kufuatia hatua ya kinara wa chama cha ANC Musalia Mudavadi kuamua kushirikiana na naibu rais William Ruto kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi agosti.
Baadhi ya wandani wa naibu rais William Ruto katika kaunti hii ya Pokot magharibi wameelezea kuridhishwa na hatua hiyo wakisema kuwa ni jeki mkubwa kwa Ruto kwani sasa atakuwa na uhakika wa kupata kura za magharibi ya nchi.
Wakazi hao wametetea hatua ya Mudavadi wakidai ni hatua yenye busara ambayo itakuwa ya manufaa kwake katika ulingo wa kisiasa, kwani wanasiasa walikuwa wakimzingira awali walinuiwa kumzubaisha kwa manufaa yao.